Sunday, July 14, 2013

VIJANA MUWE MACHO....

Hii ni kwa  vijana;

Kumbukeni kuwa wakati wa ujana ni wakati muhimu sana katika maisha ya  binadamu na ujana ukipita haurudi tena kamwe. Wakati wa ujana ndiyo wakati ufaao kwa ajili kujikusanyia elimu,mafunzo na taaluma mbalimbali zilizojazana chini ya jua letu.Vijana mnapaswa kutumia nafasi na nguvu zote kwa ajili ya kutimiza mambo yaliyotajwa hapo juu na kamwe msidanganyike na tamasha la ulimwengu ambalo linapita mithili ya tamithiliya.

Kila siku inayoitwa siku mpya machoni pa binadamu  ni siku mpya kwa maendeleo ya sayansi na  teknolojia yake  ambayo waathirika wake  wakubwa ni vijana kutokana na uwezo wenu wa kupokea na kuhifadhi maarifa mapya kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.

Wosia wangu kwenu  ni kuendelea kutumia nafasi hiyo kwa manufaa yenu; familia zenu  na maisha yenu ya kila siku. Jiandae  katika kutambua hatari zinazowakabili maishani.


Enyi vijana wa kike na kiume  tumieni mitandao kijamii kwa ajili ya kujipatia manufaa za kielimu, biashara na uchumi kwa ujumla wake na  si uwanja wa kuchokoza hisia za kimapenzi  ili kujiepusha na ngono za ujanani zinazoambatana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa chini ya hitimisho la kifo cha mapema.