Saturday, July 27, 2013

Je unataaluma hiyo?

Ni bora kukaa kimya kama hujui jambo fulani sio kulopoka mwisho wasiku utaonekana huna maana.Wakatimwingine unakuta mtu mishipa imemtoka kuongea kitu hata akijui au amesikia tena kwa mtu asiye makini alafu naye anachukua pumba hizo na kubwabwaja ovyo.Ni heri tuongelee kitu tunacho fahamu au tulicho kiona.

Vyombo vya habari na mitandao isiwe sehemu ya kuonyeshana ubabe

Vyombo vya habari au mitandao ya kijamii vitumike katika kuiendeleza jamii si vinginevyo.Watu wanatumia vibaya vyombo hivi kudhalilishana na kukebehiana.Badala ya kuombana msamaha inapo bidi lakini mnatupiana maneno sijui mnaona sifa afu mtangazaji sijui anajisikiaje au ndo kushuka kwa maadili.Sio kila mtu anafurahi kujibizana kwenu.Ebu tubadilike 

Mpaka lini tutakuwa kichwa cha mwendawazimu

Kila kitu sisi tunasuasua sio michezo,siasa,elimu wala sanaa.Tatizo kubwa ni kujuana na kuacha majembe ambayo yangesonga mbele katika nyanja za kimataifa.Utakuta mtu akianzisha kitu kizuri anasongwasongwa mpaka anakata tamaa.Hata tuzo tunapeana kwa kujuana na kusababisha kutosonga mbele.


Mungu ibariki nchi yetu.

Nani mtetezi wa wanyonge

Looh inauma napoona wanyonge tunaonewa.Kuna mambo mengi tunashindwa kupata kulingana na kipato chetu.Nguvu ya uma imekuwa hadithi katika nchi zetu.Ila kinachotuponza ni uelewa mdogo miongoni mwetu.Kuna kero nyingi sana kitaa ambazo zinashindwa kutekelezwa na viongozi wetu cha ajabu bado tunaendelea kuwachagua.Kama mtu ameshindwa kutekeleza ahadi zake bila sababu za msingi apigwe chini.

Hasira

Naamini wanadamu wote tuna hasira.Ivi kuna mtu akifinywa anaweza akawa anacheka? badala ya kugugumia maumivu.Kama sio basi ndo tulivyo umbwa .Ila utakuta baadhi ya watu wanajiona hawana hasira ki ukweli tumepishana kiwango katika kuidhibiti hiyo hasira.