Saturday, September 14, 2013

WATENDAJI WA SERIKALINI/MASHIRIKA YA UMMA WANABOA

Imekuwa kawaida sana katika taasisi,mashirika au serikalini watendaji wake kutozingatia matakwa ya wateja.Hii inatokea sana katika utoaji huduma serikalini ni ubabaishaji mkubwa utapigwa tarehe mpaka ukate tamaa.Alafu hawazingatii muda wa kazi wa kuingia kazini na wakiingia kazini hadithi nyingi badala ya kufanya huduma. Customer care imekuwa tatizo kwa hawa watendaji please tunahitaji huduma maana msipofanya ivyo mnarudisha maendeleo nyuma maana ukichelewa kunihudumia jua wazi, kazi zingine zinasimama kwasababu ya kukusubiri ww ambae umefanya serikali ni shamba la bibi..

AJIRA HAIJAWA NGUMU KIIVYO

Tumekuwa tukitishana sana eti haaa sasa ivi ajira hamna bora kujiajiri.Yawezekana ikawa sahihi ila si kwa fani zote.Vilele kujiajiri kunahitaji mtaji mtu hawezi kumaliza tu masomo yake nakujiajiri kirahisi labda kama ni kuuza karanga au ufundi baiskeli.Lakini kama umemaliza shahada  mtu utapenda ufanye biashara kubwa.Ni kweli kunachangamoto ya kuajiriwa ila sio kiasi inavyosemwa na wengi ila ni sera mbovu ya serikali ndio chanzo cha yote haya.Maana nchi hii inaviwanda na mashirika mengi tatizo ni uendeshaji wa mashirika hayo ambayo hayazingatii taratibu za wafanyakazi kwa lengo lakujipatia faida kubwa.

Masista du

Madada wengine wanashangaza sana wanamapozi mpaka wanaboa.Unakuta dada analeta pozi utadhani labda yeye ni special sana.Utu wetu sote ni sawa mtu asijione kama yeye ndio yeye mambo yanabadilika muda wowote.Sana madada wa dzm wamesahau duniani kila mtu anapenda maisha mazuri labda kama mtu atakuwa punguani ndio anaweza asipende vitu hivi.Mapozi yamezidi sana wakati mwingine umbo baya,sura mbaya hata mvuta hana ila maringo yamezidi.Hata kama ww ni mzuri si kila mtu labda anababaika na ww kikubwa ni kujirekebisha.

Vyombo vya habari

Waandishi wengi wa kibongo wamekuwa wakitukosesha haki ya kupata habari sahihi.Hii inatokana na uoga au itikadi zao za kutetea maslai binafsi.Inapoteza matumaini kama tabia hii itaendelea bila ufumbuzi maana itatengeneza taifa lisilokuwa na watu wenye weledi wa kuelewa mazingira yao kiuchumi,kisiasa hata kisayansi maana hawana maelezo sahihi ya habari zilizopo,zilizopita au zinazo endelea.