Sunday, July 28, 2013

Si sahihi

Mtazamo huu si sawa eti ukiongea ukweli utachukiwa.Hii aileti maana kwasababu tukikubaliana hivyo basi inamaana watu wanapenda kudanganywa.Msemo huu unatumika pale tu kunapo kuwa na maslahi ya watu alafu useme kweli hapo watu hao lazime wakuchue na siyo wanakuchukia kwa kusema ukweli bali  kwasababu utawahatarishia maslahi yao.Huu ndo ukweli wenyewe utaupata hapahapa tu.

Mtazamo tu

Nchi yetu sasa si nchi ile ya mwaka 47.Kwasasa Viongozi wanatakiwa wakipewa wizara basi ilingane na taaluma yake hii itasaidia utendaji bora.Huu si wakati wa ujanja ujanja hata kama unafanyika ila mwisho wake upo tu.Unapopewa dhamana na wananchi basi wajibika mbona rahisi tu.Fanya vizuri nawe ukumbukwe kama Nyerere hata kama upendi ivyo basi fanya kwasababu Mungu anaona ambavyo binadamu hawezi ona.

Freemason

Watu wengi wanaongea kuhusu freemason ila wengi hatujui ni nini?.Wapo wanasema freemason ni dini.Yawezekana ikawa ni dini ila kwa nilivyo chunguza Freemason kwa kiswahili maana yake ni Mjenzi huru.Maana yake kuna uhuru wa kuanzisha unachokitaka yaani kujenga.Jumuiya hii ni yasiri ndo maana kwa nchi za afrika haijulikani sana kama nchi za ulimwengu wa kwanza.Kiukweli jumuiya hii ni hatari sana kwa mwanadamu maana malengo yake si mazuri kwa mwanadamu.Huu ni ujanja wa shetani wa kumpa uwezo mwanadamu ili amdanganye ili waende pamoja motoni(ziwa la moto).Muovu huyu akaacha kiti chake na kumpa mwanadamu kiti hicho ili kufanya lolote amdanganye binadamu huyu.Freemason hawa wanaamini kuwa kuna nguvu ipo tu kiasili(supreme being) huyu ndo shetani kapotosha badala ya kuamini Mungu anapotosha kwamba yeye ndo ananguvu loooh Eeee Mungu utusaidie maana duniani tunayodhiki.