kama ni sheria bora duniani ni usalama barabarani.Sheria hii ya usalama barabarani ikifuatwa itasaidia sana.Lakini nchi yetu ubabaishaji mtupu kwa mfano gari la abiria tsh 400/= ila kwa sababu tu usafiri ni tabu mtalipa buku.Sawa kwa wakati huu usafiri ni mgumu utakuta watu wenye magari binafsi sio ya abiria wanakupiga kutoka 600 mpaka 2000 utafanyaje na sisi ndo wenye shida tunalipa ila sheria haijafanya kazi yake.Sio siri inaumiza sana maisha yenyewe bongo yako wapi wenye nacho watazidi kuwa nacho tu sisi wengine tutaendelea kusanda.
Hii ni kwa vijana;
Kumbukeni kuwa wakati wa ujana ni wakati muhimu sana katika maisha ya binadamu na ujana ukipita haurudi tena kamwe. Wakati wa ujana ndiyo wakati ufaao kwa ajili kujikusanyia elimu,mafunzo na taaluma mbalimbali zilizojazana chini ya jua letu.Vijana mnapaswa kutumia nafasi na nguvu zote kwa ajili ya kutimiza mambo yaliyotajwa hapo juu na kamwe msidanganyike na tamasha la ulimwengu ambalo linapita mithili ya tamithiliya.
Kila siku inayoitwa siku mpya machoni pa binadamu ni siku mpya kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yake ambayo waathirika wake wakubwa ni vijana kutokana na uwezo wenu wa kupokea na kuhifadhi maarifa mapya kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Wosia wangu kwenu ni kuendelea kutumia nafasi hiyo kwa manufaa yenu; familia zenu na maisha yenu ya kila siku. Jiandae katika kutambua hatari zinazowakabili maishani.
Enyi vijana wa kike na kiume tumieni mitandao kijamii kwa ajili ya kujipatia manufaa za kielimu, biashara na uchumi kwa ujumla wake na si uwanja wa kuchokoza hisia za kimapenzi ili kujiepusha na ngono za ujanani zinazoambatana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa chini ya hitimisho la kifo cha mapema.