Monday, September 16, 2013

Mambo ya kuzingatia ilikuwakaribu na watu

Ili mambo yako yawe mazuri ni bora zaidi maelewano ya ndugu,jamaa na marafiki yawe ya kiwango kikubwa.Yafuatayo ni mambo machache ya kzingatia ili kufanikisha jambo hili
(1)Penda kuongelea maslahi ya wengi kuliko maslahi binafsi.
(2)Jitahidi kutabasamu unapoongea na mtu au watu 
(3)Jitahidi kukumbuka jina la mtu au watu unapowasiliana nao.
(4)Wakati mwingi kuwa msikilizaji na pendelea kuimiza watu wajiongelee wenyewe, itasaidia kuwajua zaidi wanachopenda au kuchukia
(5)Fanya watu wengine wajione ni muhimu na kuwapa moyo kwa kila jambo

Sunday, September 15, 2013

Mashirika yanayotoa ajira bila ubabaishaji tanzania

Ifuatayo ni orodha ya mashirika,taasisi au ngo ambazo hazina uchakachuaji katika kutoa ajira/nafasi za kazi..

Imekuwa ni kawaida mashirika kutangaza ajira eti kwa sababu ya shinikizo la serikali kufanya hivyo.Kama ni ndio basi ni kitu kibaya sana maana ni kupotezeana muda na gharama unazowezakutumia katika ufuatiliaji ya interview au usaili.Orodha ni
(1)Aluminium Africa Limited-Nyerere road hichi ni kiwanda kinahusika na uzalishaji wa mabati
(2)Mantrac Tanzania-Nyerere road hawa wanahusika na mashine za katapila
(3)Kilombero Sugar Company Limited-Morogoro ni kiwanda cha uzalishaji sukari tanzania
(4)Nafasi mbalimbali zinazosimamiwa na Utumishi
(4)TANROAD
(5)Central Electrical International-Hawa ni wanahusika na wiring katika miradi mikubwa ya nyumba/maghorofa ya mashirika binafsi au ya UMMA
(6)Radi Services-Bagamoyo road ni wataalamu wa mashine za motor,transformer na generator
(7)Tanga cement-Tanga watengenezaji wa cement
(8)Mtibwa sugar-Morogoro wanahusika na uzalishaji wa sukari
(9)Tanalec Arusha-Wasukaji wa transformer
(10)Muhimbili National Hospital
(11)Delta-Nyerere road
(12)CSI

Saturday, September 14, 2013

WATENDAJI WA SERIKALINI/MASHIRIKA YA UMMA WANABOA

Imekuwa kawaida sana katika taasisi,mashirika au serikalini watendaji wake kutozingatia matakwa ya wateja.Hii inatokea sana katika utoaji huduma serikalini ni ubabaishaji mkubwa utapigwa tarehe mpaka ukate tamaa.Alafu hawazingatii muda wa kazi wa kuingia kazini na wakiingia kazini hadithi nyingi badala ya kufanya huduma. Customer care imekuwa tatizo kwa hawa watendaji please tunahitaji huduma maana msipofanya ivyo mnarudisha maendeleo nyuma maana ukichelewa kunihudumia jua wazi, kazi zingine zinasimama kwasababu ya kukusubiri ww ambae umefanya serikali ni shamba la bibi..

AJIRA HAIJAWA NGUMU KIIVYO

Tumekuwa tukitishana sana eti haaa sasa ivi ajira hamna bora kujiajiri.Yawezekana ikawa sahihi ila si kwa fani zote.Vilele kujiajiri kunahitaji mtaji mtu hawezi kumaliza tu masomo yake nakujiajiri kirahisi labda kama ni kuuza karanga au ufundi baiskeli.Lakini kama umemaliza shahada  mtu utapenda ufanye biashara kubwa.Ni kweli kunachangamoto ya kuajiriwa ila sio kiasi inavyosemwa na wengi ila ni sera mbovu ya serikali ndio chanzo cha yote haya.Maana nchi hii inaviwanda na mashirika mengi tatizo ni uendeshaji wa mashirika hayo ambayo hayazingatii taratibu za wafanyakazi kwa lengo lakujipatia faida kubwa.

Masista du

Madada wengine wanashangaza sana wanamapozi mpaka wanaboa.Unakuta dada analeta pozi utadhani labda yeye ni special sana.Utu wetu sote ni sawa mtu asijione kama yeye ndio yeye mambo yanabadilika muda wowote.Sana madada wa dzm wamesahau duniani kila mtu anapenda maisha mazuri labda kama mtu atakuwa punguani ndio anaweza asipende vitu hivi.Mapozi yamezidi sana wakati mwingine umbo baya,sura mbaya hata mvuta hana ila maringo yamezidi.Hata kama ww ni mzuri si kila mtu labda anababaika na ww kikubwa ni kujirekebisha.

Vyombo vya habari

Waandishi wengi wa kibongo wamekuwa wakitukosesha haki ya kupata habari sahihi.Hii inatokana na uoga au itikadi zao za kutetea maslai binafsi.Inapoteza matumaini kama tabia hii itaendelea bila ufumbuzi maana itatengeneza taifa lisilokuwa na watu wenye weledi wa kuelewa mazingira yao kiuchumi,kisiasa hata kisayansi maana hawana maelezo sahihi ya habari zilizopo,zilizopita au zinazo endelea.