Sunday, July 14, 2013

TUFUATE UTARATIBU..

Wakati mwingine nakereka sana.. Utakuta mtu kwenye mtandao wa kijamii  eti anaandika inrelationship ina maana gani  sasa tena anakuacha njia panda bora kidogo aandike inrelatioship with somebody kiasi fulani ina mantiki.Ila bora zaidi kuandika Engaged au married.

HAPO TUTAENDA SAWA..

HIVI DUNIANI HAPA TUPO KWA KUSUDI GANI??

Kila nikijiuliza kusudi la kuepo duniani napata kigugumizi .Je tumekuja kujitesa au kupingana na maumbile halisi ya kibinadamu..Ndio kwa sababu vitu vizuri vingi ni haramu au wanasema anasa.Kwa mifanano Moja ni pombe hii inapendwa na baadhi ya jamii na ni sehemu ya kiburudisho kwao;Pili ni Wanawake/Wanaume hawa wanapingwa sana ila unatakiwa kuwa naye mmoja hasa baada ya ndoa na Tatu Chakula unakuta watu wanajinyima kula eti wamefunga..

Lakini baadhi ya ivyo vina leta maana Mfano POMBE kiukweli ukizidisha pombe lazima utafanya mambo ya ajabu nakukusababishia Majuto; na Pili Wanawake/Wanaume kimsingi tukiwa waaminifu kwa kuwa na mke/mme mmoja tutaishi kwa amani na kujiamini ila ukienda tofauiti tuu inakula kwako mara eeh kaswende ,gonorhea mbaya zaidi UKIMWI.Ila hata kula kwaweza sababisha madhara mfano baadhi ya vyakula watu wana aleji navyo.Ndo maana katika uzima wa milele hakuna kula wala kunywa.

HAAAA KILA KITU DUNIANI KINAMAKUSUDI YAKE.

BINADAMU TUSHIRIKIANE.

Wakati mwingine sisi binadamu ni waajabu sana.Badala yakufikilia maisha haya tutafanyaje yawe nafuu kwa kila mtu lakini unakuta mtu anapindisha tu eti kwa kulinda itikadi zake.Dunia mapito jombaa tushirikiane kama mchwa tufike lengo..Maana utanicheka mimi leo kesho yanaweza mkuta ndugu,rafiki au kizazi chako mwenyewee..

VIJANA MUWE MACHO....

Hii ni kwa  vijana;

Kumbukeni kuwa wakati wa ujana ni wakati muhimu sana katika maisha ya  binadamu na ujana ukipita haurudi tena kamwe. Wakati wa ujana ndiyo wakati ufaao kwa ajili kujikusanyia elimu,mafunzo na taaluma mbalimbali zilizojazana chini ya jua letu.Vijana mnapaswa kutumia nafasi na nguvu zote kwa ajili ya kutimiza mambo yaliyotajwa hapo juu na kamwe msidanganyike na tamasha la ulimwengu ambalo linapita mithili ya tamithiliya.

Kila siku inayoitwa siku mpya machoni pa binadamu  ni siku mpya kwa maendeleo ya sayansi na  teknolojia yake  ambayo waathirika wake  wakubwa ni vijana kutokana na uwezo wenu wa kupokea na kuhifadhi maarifa mapya kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.

Wosia wangu kwenu  ni kuendelea kutumia nafasi hiyo kwa manufaa yenu; familia zenu  na maisha yenu ya kila siku. Jiandae  katika kutambua hatari zinazowakabili maishani.


Enyi vijana wa kike na kiume  tumieni mitandao kijamii kwa ajili ya kujipatia manufaa za kielimu, biashara na uchumi kwa ujumla wake na  si uwanja wa kuchokoza hisia za kimapenzi  ili kujiepusha na ngono za ujanani zinazoambatana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa chini ya hitimisho la kifo cha mapema.






WAHENGA WALISEMA

Kuishi kwingi kuona mengi... Kila siku binadamu maarifa yana ongezeka..So tueshimiane sana sio unamuona mwenzako unamchukulia hopeless hasa mtu haumjui..